WAFANYAKAZI WANAWAKE WATAKIWA KUENDELEA KUKAMATA FURSA YA ELIMU ILI KUFIKIA MALENGO YAO

7 Machi 2024, DAR ES SALAAM

Wafanyakazi wanawake nchini wametakiwa kuweka katika vipaumbele vyao suala ya kujiendeleza kielimu ili kuweza kuleta mabadiliko katika sehemu zao za kazi sambamba na kujiimarisha kiuchumi.

Wito huo umetolewa na Mbunge wa Viti Maalumu anayewakilisha Wafanyakazi Mhe. Janejelly James Ntate ( MB) leo Alhamis tarehe 7 Machi 2024 alipokuwa Mgeni Rasmi katika Kongamano kubwa la Wafanyakazi Wanawake lililoandaliwa na Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania ( TUCTA).

Mhe. Ntate amesema kuwa ili kuharahisha maendeleo katika taifa na Jamii kama ambavyo kauli mbiu ya mwaka huu imehimiza , ni lazima kufanya uwekezaji mkubwa kwa Wanawake ikiwemo kuwaendeleza kielimu ili waweze kuleta tija na kuwa na chachu ya mabadiliko katika Sehemu zao za kazi.

Sambamba na wito huo pia amewataka wanawake kupendana, kushirikiana katika mambo mbalimbali pia wasifungie vipawa vyao ndani naye kwa upande wake kupitia nafasi yake ataendelea kuwawakilisha vyema bungeni kwa kuzisema hoja mbalimbali za Wafanyakazi anapokuwa Bungeni.

Akimkaribisha Mgeni Rasmi Mwenyekiti wa Wanawake TUCTA, Ndg. Rehema…….amevishukuru Vyama vyote vinavyounda Shirikisho hilo la Wafanyakazi kwa kushiriki kikamilifu katika Kongamano hilo na kuwataka kutumia kongamano hilo kujadiliana na kujiwekea malengo yenye Tija ili kuleta mabadiliko katika Vyama vyao na baadae kwenye Shirikisho

Kongamano hilo limehudhuriwa na Wawakilishi kutoka katika Vyama vya Wafanyakazi vinavyounda Shirikisho hilo ikiwa ni sehemu kuelekea katika kilelele cha Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani kwa mwaka huu ambapo kilele chake kitakuwa ni kesho Machi 8.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *